Sera ya Faragha (Privacy Policy)

1. Utangulizi

WitoPlus ("sisi", "yetu") imejitolea kulinda faragha yako. Sera hii ya Faragha inaelezea jinsi tunavyokusanya, kutumia, na kulinda habari zako unapotumia mfumo wetu wa kadi za kidijitali na usimamizi wa matukio.

2. Taarifa Tunazokusanya

Tunakusanya taarifa ambazo ni muhimu tu kwa ajili ya kutoa huduma zetu:

  • Taarifa za akaunti (Jina, barua pepe, namba ya simu).
  • Taarifa za matukio (Majina ya maharusi/wenye shughuli, tarehe, na mahali).
  • Orodha ya wageni (Majina na namba za simu kwa ajili ya kutuma kadi).

3. Jinsi Tunavyotumia Taarifa Zako

Taarifa zako zinatumika kwa madhumuni yafuatayo:

  • Kutengeneza na kutuma kadi za kidijitali.
  • Usimamizi wa mahudhurio (RSVP) na michango (Mkeka).
  • Mawasiliano kuhusu akaunti yako au mabadiliko ya huduma.

4. Kushiriki Taarifa (Third Parties)

Sera yetu ni madhubuti: Hatuziuzi, hatuzikodishi, wala hatushiriki taarifa zako binafsi au za wageni wako na makampuni ya nje kwa ajili ya matangazo au biashara nyingine yoyote.

5. Usalama wa Data

Tunatumia mifumo ya kisasa ya ulinzi wa kidijitali kuhakikisha kuwa taarifa zako zipo salama dhidi ya ufikiaji usioidhinishwa.

6. Mawasiliano

Ikiwa una maswali yoyote kuhusu sera hii, tafadhali wasiliana nasi kupitia barua pepe yetu rasmi.

Mwisho wa kufanyiwa marekebisho: March 15, 2026